Wednesday, June 1, 2011

UZINDUZI WA VIDEO YA "NILIPE NISEPE" NDANI YA CLUB BILCANAZ

Jumapili hii Belle 9 atazindua Video yake mpya ya NILIPE NISIPE pale Club Bilcanaz huku akisindikizwa na wasanii wenzake wa kizazi kipya Quik Rocka & Linex...pia Belle 9 atakamua ngoma zake zote kama Sumu ya penzi,Masogange,We ni Wangu na nyingine kibaoooo.....

Tuesday, May 31, 2011

SERENGETI FIESTA FREESTYLE 2011 MADADASHOSTI NAO WAMO!!!!

2PAC YU HAI?

Uzushi mwingine ulikuwa ni wa mtu mzima 2pac ambae alifariki dunia mwaka 1996
kama uliingia chaka na kukubali utakua mjinga, ilifikia mpaka idadi wa watu 3,000 waliingia chaka juu ya story iliyokua ikitapakaa kila sehemu ambayo ilikua ikisema tupac yuko hai na anaishi New Zealand..
   

WILL SMITH: KAFARIKI DUNIA?

story zilizotanda kila kona ya kuwa Will Smith msanii, muigizaji na mchekeshaji amefariki kwa kuji overdoze, zimekanushwa na website mbali mbali na kudai kuwa ni uzushi tu, na si mara ya kwanza kuzushiwa kwa Will Smith ambapo mwaka jana alizushiwa kuwa amefariki kwa ajali ya gari. will smith yupo kitaa bado anaendelea kupeta kitaa na kukisanua kama kawa

WAKACHA WASHADONDOSHA PINI JIPYA

Wakacha kundi linaloundwa na jamaa wenye swagga  za hatari wameshadondosha pini jipya linaloitwa Here we go chini ya producer Pancho Latino...................

PACHA WA P-SQUARE AVAMIWA NA MAJAMBAZI

Mmoja wa pacha wanaounda kundi la P-Square,Paul Okoye alionja joto ya jiwe baada ya kuvamiwa na majambazi alipokuwa njiani kuelekea Victoria Island kucheki washikaji zake Paul alikuwa akiendesha mkoko wake mpya aina ya BMW X6 lenye plate number za "RUDE BOY"na kwa moyo wa utu aliokua nao ndio uliomponza,coz alisimama njiani kutoa msaada kwa waliopata ajali na watu wawili kutokea pasipojulikana na kumtolea bastola na kumpora simu,fedha na vito vya thamani na vinginevyo.........

A .Y NEXT LEVEL!!

AMBWENE YESSAYAH A.K.A A.Y  Mzee wa Commercial amekwenda next level zaidi baada ya kufanya collabo na mkali kutoka marekani,Percy Romeo Miller JR. aka Lil Romeo na D'anna Stewart,ngoma iitwayo Speak with your Body.....Mbali na Lil Romeo pia kwa sasa ana mpango wa kufanya kazi na Soulja Boy,coz aliacha demo yake na baada ya Soulja Boy kuisikia collabo na Lil Romeo alizima makila kinga ya AY na kuamua kufanya nae kazi na kwa sasa AY anasubiri aletewe beats tu azifanyie kazi na mwezi ujao anatarajiwa kwenda Marekani kwa ajili ya kupiga huo mzigo pamoja na kutengeneza video ya Speak with your Body